Uwanja huo wa Arena da Baixada katika jiji la Curitiba ulipangiwa kuchezwa mechi nne za kombe la dunia. Ukarabati wa uwanja huo ulikwishacheleweshwa kwa kipindi kadhaa.
Jaji Lorena Colnago alisema maisha ya wafanyikazi yanahatarishwa kutokana na hali ya kuzorota kwa ujenzi huo. Akiongeza kusema kuna hatari ya kuzikwa,kukanyagwa na magari na hata kudondoka kutoka kuta za juu za uwanja huo.
Aliamrisha ukaguzi mpya ufanywe kabla ya kuanza tena shughuli za ujenzi. Akiongeza kusema kumegunduliwa kasoro nyingi katika ujenzi huo.
Taarifa hizo zinakuja wiki moja tu baada ya uchunguzi kufichua kwamba wafanyikazi walioajiriwa katika ujenzi wa mradi mwingine wa kombe la dunia walikabiliwa na hali ya kitumwa.
Wachunguzi hao walisema pia kwamba zaidi ya wafanyikazi 100 walioajiriwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sao Paulo wanaishi katika hali duni karibu na uwanja huo.
Mnamo mwezi wa Agosti, waziri wa michezo Aldo Rebelo alisema ana wasiwasi jinsi ujenzi ulivyochelewa katika viwanja vitano vya michuano ya kombe la dunia mwakani.
Baada ya ziara yake nchini Brazil, katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke,alisema viwanja vyote lazima viwe tayari ifikapo mwezi Desemba na kuonya hatavumilia tena kuchelewesha ujenzi na hakuna 'mpango mbadala'.
Michuano ya kombe la dunia imepangwa katika viwanja 12 nchini kote Brazil.
0 comments:
Post a Comment