Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, February 19, 2014

Wyre Kupambana na Jay Z,50 Cents,Asap Rocky na Pharell kwenye World Music Awards



Mkali wa miondoko ya Reggae na R&B kutoka Kenya, Wyre the Love Child, anaendelea kufanya vizuri na kupaisha vizuri Afrika Mashariki ambapo mwaka jana 2013 aliweza kuibuka mshindi katika kipengele cha "Best New Entertainer – Wyre" kwenye tuzo za International Reggae and World Music Awards (IRAWMA) zilizofanyika huko Lauderdale, Florida. 
Kazi za Wyre zimeendelea kufanya vizuri pia mwaka huu na kuvuka zaidi kimataifa na kumpelekea kuwa nominated katika tuzo zenye uzito wa hali ya juu za World Music Awards (WMA) katika kipengele cha World Music Artiste na kikubwa zaidi ni ameshindanishwa na wasanii nguli katika music duniani akiwemo Jay Z,50 Cent,Asap Rocky,Pharell na wengine wengi.. Hii inaonyesha wazi kukuwa kwa muziki wa Afrika Mashariki na kueleweka Duniani kote.. 

Tuesday, February 18, 2014

Bebe ajipanga kuonyesha maajabu kwenye kazi zake mpya


Msanii Bebe Cool, ameamua kuwekeza nguvu ya kutosha katika kazi zake mpya, ambapo ameonekana akitumia vifaa vya kisasa kabisa katika kutengeneza video yake mpya ya ngoma inayofahamika kama Nkola Byafaayo.

Katika video hii, Bebe Cool ameonekana kujipanga vilivyo kuanzia mavaazi yake location mpaka aina za kamera alizotumia kwaajili ya kuleta maana halisi ya jina la wimbo huu kwa kiswahili, Nkola Byafaayo, 'fanya maajabu'.

Bado msanii huyu hajaweka wazi kitita cha pesa alichounguza kufanya video hii, ila amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa itakamilika hivi karibuni tayari kwa kuwachangaza na kuwaburudisha.

Monday, February 17, 2014

Ejiofor Atwaa Tuzo Toka BAFTAs


Muigizaji wa filamu Chiwetelu Umeadi maarufu kama "Chiwetel Ejiofor" ameendelea kufanya vizuri katika ulimwengu wa filamu dunia baada ya kutwaa  tuzo katika British Academy Film Awards 2014 "BAFTA" zilizofanyika jana katika ukumbi wa London Royal Opera House, katika filamu ya '12 Years a Slave' katika kipengele cha leading Actor at the 2014 BAFTAs.

Hii ndio list nzima ya washindi wa tuzo hizo...
  • Best Film Winner: 12 Years A Slave
  • Leading Actress Winner: Cate Blanchett (Blue Jasmine)
  • Director Winner: Alfonso Cuaron (Gravity)
  • Leading Actor Winner: Chiwetel Ejiofor
  • Film Not in the English Language Winner: The Great Beauty
  • Special Visual Effects Winner: Gravity
  • EE Rising Star Winner: Will Poulter
  • Adapted Screenplay Winner: Philomena
  • Original Screenplay Winner: American Hustle (Eric Warren Singer, David O. Russell)
  • Outstanding British Contribution to Cinema Winner: Peter Greenaway
  • Supporting Actress Winner: Jennifer Lawrence
  • Cinematography Winner: Gravity
  • Supporting Actor Winner: Barkhad Abdi (Captain Phillips)
  • Outstanding Debut by a British Writer, Director or Producer Winner: Kieran Evans (Kelly + Victor)
  • Animated Film Winner: Frozen
  • Original Music Winner: Gravity
  • Costume Design Winner: The Great Gatsby
  • Make-Up and Hair Winner: American Hustle
  • Documentary Winner: The Act Of Killing
  • Editing Winner: Rush
  • Fellowship Winner: Dame Helen Mirren

Thursday, February 13, 2014

[Photos] TAZAMA MAGARI YA GOOGLE YASIYO NA DEREVA

Hizi ni baadhi ya Gari mpya toka Google ambazo zimekuja na teknolojia mpya ya kujiendesha zenyewe bila kuwa na dereva.
Tazama baadhi ya picha za gar hizo..








KILI MARATHON 2014 MBIONI KUANZA


Shindano la mbio za Kilimanjaro Marathon 2014 liko mbioni kuanza Machi 2014, huku waandaaji wa shindano hilo wakiwa wameongeza zawadi zaidi ya Sh milioni 40 kwa washindi wa shindano hilo na kuzifanya mbio hii kuwa kati ya mbio kubwa zaidi barani Afrika..
Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers,ambao pia ni waandaaji wa shindano hilo, John Addison alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa mbali na zawadi hiyo ya fedha, washindi pia watajishindia zawadi nyingine nono kutoka kwa wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na wadhamini shirikishi.
Addison alisema washindi wa mbio ndefu za marathoni za kilometa 42, watajishindia Sh milioni 20, na zawadi ya fedha taslimu Sh milioni 10 kwa washindi wa nusu marathon huku washindi wa mbio za walemavu maarufu kama GAPCO 10km Marathon wakijishindia Sh milioni sita.
Washiriki wote watakaomaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watajishindia zawadi mbalimbali. Alisema mbio za mwaka huu zimesheheni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki.
Washindi wa kwanza katika marathoni wanawake kwa wanaume watajinyakulia Sh milioni 4 kila mmoja, Sh milioni 2 kwa washindi wa pili na Sh milioni 1 kwa washindi wa tatu.
Washindi wa kwanza katika nusu marathoni wanawake kwa wanaume watapewa Sh milioni mbili kila mmoja, Sh milioni 1 kwa washindi wa pili na Sh 500,000 kwa washindi wa tatu.
Addison alisema medali na fulana zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilometa 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu.
“Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa fulana baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za kuvutia kupitia droo,” alisema mkurugenzi huyo.
Ili kuwapa hamasa wanariadha wa Tanzania kufanya vizuri katika mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager imetenga Sh milioni mbili kama bonasi kwa wanariadha Watanzania watakaovunja rekodi katika mbio hizi.
Mbio hizo zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.

Wednesday, February 12, 2014

Kikosi cha Azam Fc Kimeelekea Msumbiji Kuikabili Ferroviario de Beira

MSAFARA wa watu 37 wa klabu ya soka ya Azam leo umeelekea mjini Beira nchini Msumbiji, kuikabili Ferroviario de Beira katika mechi ya pili ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam FC itarudiana na timu hiyo ya Msumbiji, Jumamosi wiki hii baada ya kuwa timu hizo zilimenyana juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na wenyeji kushinda kwa bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na nyota wa Ivory Coast, Kipre Tchetche. Ili kusonga mbele katika hatua ya kwanza, vijana hao wa Joseph Omog, watapaswa kuhakikisha hawafungwi, badala yake wapate sare ya aina yoyote au ushindi.
Kwa mujibu wa Meneja wa Azam FC, Jemedari Said, kikosi cha timu hiyo kitakuwa na wachezaji 21 na viongozi 16 wakiwamo wa benchi la ufundi na viongozi wa klabu hiyo inayoshiriki michuano hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.
Wachezaji waliyounda kikosi hicho kilichosafiri leo ni Mwadini Ali, Aishi Manula, Jackson Wandwi, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Luckson Kakolaki, Aggrey Morris, Said Morad, Kipre Bolou, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz na Himid Mao.
Wengine ni Salum Abubakar, Seif Abdallah, Kipre Tchetche, Brian Umony, Kone Ismail, Gaudence Mwaikimba, Mcha Khamis Mcha, David Mwantika na John Bocco.
Na hili ndio benchi la ufundi linaloundwa na  Kocha Mkuu Omog, raia wa Cameroon, makocha wasaidizi, Kally Ongalla na Ibrahim Shikanda, Kocha wa Vijana, Idd Cheche, Daktari Juma Mwankemwa, Daktari wa viungo Vicent Madege na Mtunza Vifaa Yussuf Nzawila.
Wengine ni Katibu Mkuu wa klabu, Idrisa Nassoro, Ofisa wa Itifaki, Abubakar Mapwisa, Jamal Bakhresa, Msemaji wa Azam Media, Florian Kaijage na Jaffar Maganga na Kassim Khan pia kutoka Azam Media.
Picha za Timu ya AZAM wakiwa uwanja wa ndege kabla ya safari yao kuelekea mjini Beira nchini Msumbiji.





Tuesday, February 11, 2014

[Photo's] Filamu Mpya Toka kwa Lupita Nyong'o

Lupita Amondi Nyong'O ni Muigizaji na Muongozaji wa filamu toka nchini Kenya, alizaliwa  Machi 1, 1983. Muigizaji huyu aliyetamba na filamu kama “12 Years a Slave” iliyobamba na kumpatia umaarufu zaidi mwaka 2013 pamoja na kumpatia tuzo, hivi sasa yupo mbioni kuachia filamu yake mpya Februari 28.

Hizi ni baadhi ya picha kwenye Movie yake mpya..




Tatoo's Mpya za Jose Chameleone


Mwanamuziki wa mkali toka Uganda Jose Chameleone  hitmaker wa Valu Valu,Badilisha na Tubonge ambaye kwa sasa yupo South Africa kwenye ziara yake ya kimuziki,ameamua kuwa surprise mkewe ‘Daniela’ na watoto wake kwa kipekee kwa kuchora tattoo mwilini mwake.
Jose Chameleone alifunguka haya baada ya kujichora tattoo hizo.. ”2014 we stand tall for the ones we care for and those that love us back with their whole” 

 Hizi ndio picha za Tatoo alizochora Chameleone..

[New Music] Wiz Khalifa - We Dem Boyz

Sikiliza Ngoma mpya ya Wiz Khalifa-We Dem Boyz kupitia link hii http://viewhiphop.com/71192

Wednesday, February 5, 2014

BALOTELLI NDANI YA MUONEKANO MPYA

Mshambuliaji wa Kiitaliano anayeichezea klabu ya Serie A ya AC Milan Mario Balotelli ameendelea kushikilia vichwa vya habari baada ya ku'share picha ya mtindo wake mpya wa kunyoa nywele.

Balotelli alipiga picha akiwa salon mara baada kumaliza kunyolewa mtindo mpya na kinyozi wake AMOS na kuanza ku'share kwa mashabiki wake mtindo mpya huo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akimsifia kinyozi wake AMOS kwa kazi nzuri aliyoifanya na kuandika ndiye kinyozi bora kwa upande wakekwa kuandika maneno haya kwenye tweet yake...

Matokeo ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Ikiwa ni muendelezo wa mzunguko wa pili katika mchezo wa mpira wa miguu kwenye Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, haya ni matokeo ya mechi zilizochezwa leo february 5 katika viwanja tofauti tofauti.

Tuesday, February 4, 2014

Chelsea Yaichapa Man City

Ikiwa ni muendelezo Ligi ya Uingereza,jana kulikuwa na mechi ngumu kati ya Manchester City V Chelsea. Chelsea walitoka kifua mbele kwa kuchalaza Man City bao moja kwa bila huku wakiwa wamevunja rekodi ya Manchester City kushindwa kufunga bao katika mechi za nyumbani tangu mwaka 2010.
Bao la Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic dakika ya 32' katika kipindi cha kwanza. Huku mchezaji Nemanja Matic akiwa ndo 'Man of The Match'
Kutokana na mechi hiyo Manchester City na Chelsea zina alama sawa lakini Mancity imefunga mabao mengi.