Wednesday, October 9, 2013
JANUZAJ AWAPASUA KICHWA MAN UNITED, BARCA WANA UHAKIKA WATAMNASA.
Fc Barcelona iko tayari kumchukua Adnan Januzaj kutoka Manchester United iwapo atakataa ofa ya aliyotengewa sasa na Manchester United ya kuongeza mkataba wake wa sasa kabla haujafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland Jumamosi iliyopita....
Lakini Barca imekuwa ikifuatilia kipaji cha mwanasoka huyo tangu hajajiunga na United kutoka Anderlecht mwaka 2011. Barca wana imani kwamba hata iweje Januzaj ataishia kuhamia Nou Camp wakati atakapomalizia miezi minane iliyobaki katika mkataba wake na United.
Mbelgiji siku za hivi karibuni alisema ana furaha kuwepo United, lakini imeelezwa kwamba kuna wakati alihisi kutokuhitajika klabuni hapo.
Mazungumzo ya mkataba mpya yalikuwepo pindi meneja mstaafu, Sir Alex Ferguson hajaachia ngazi Mei mwaka huu na tokea kipindi hicho baba wa Januzaj amekua akifuatilia kwa karibu kutaka mwanae apewe mkataba mpya bilamafanikio yoyote kitu alichotafsiri kua mtoto wake haitajiki klabuni hapo.
Baba wa Januzaj ana kauli zaidi hata ya ajenti wa kinda hyuo aitwaye De Vriese na hata Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Anderlecht, Jean Kindermans, mtu ambaye anastahili sifa za kuibua kipaji hicho, alionya jana usiku kwamba Januzaj Snr anataka kuwa na kauli ya mwisho juu ya mwanaye kama atabaki United au ataondoka na pia juu ya timu ipi ya taifa ataichezea.
Akiwa amezaliwa Ubelgiji na wazazi Kosovo na Albania, Januzaj anaweza kuchezea nchi kadhaa na kocha wa Ubelgiji, Marc Wilmots amechukua hatua ya kwanza kwa kumuita mchezaji huyo kikosini mwake kwa ajili ya mechi zijazo za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Croatia na Wales.
Lakini ombi hilo lilikataliwa, huku Januzaj akiwataka mabosi wa Old Trafford kujibu kwamba anataka muda zaidi wa kufikiria mustakabali wa utaifa wake.
Januzaj alisema: "Kwa sasa, soka ya kimataifa si jambo ninalofikiria kwa kiasi kikubwa. Nafahamu kwamba, kwanza natakiwa kuelekeza fikra zangu juu ya kile ninachokifanya United, kwa sababu hiyo ndiyo muhimu zaidi katika soka yangu kwa sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment