Taarifa ikufikie kwamba aliekua daktari wa mwimbaji staa wa Pop
duniani Michael Jackson, Conrad Murray ameachiwa huru kutoka jela baada
ya kutumikia kifungo kwa miaka miwili kati ya minne aliyokua amehukumiwa
kutokana na kifo cha MJ mwaka 2009.
CNN wameripoti kwamba Daktari huyu ilibidi atumie mlango mwingine
kutoka jela ili kukwepa waandishi wa habari pamoja na baadhi ya
mashabiki wa Michael Jackson wenye hasira waliokuwemo nje ya jela baada
ya kupata taarifa kwamba anatolewa kwenye jela hiyo ya Los Angeles.
Mwanasheria wake amekaririwa akisema kwamba Doctor Conrad anaweza
kurudi kuendelea na kazi yake ya udaktari lakini moja kati ya kauli za
familia ya Michael Jackson ni ‘ni wazi kwamba Conrad ndio alimuua
Michael Jackson, tunamatumaini kwamba hatofanya udaktari tena na
kumuumiza wengine’
Tuesday, October 29, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment