Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, October 4, 2013

Tottenham yang'aa kwenye Uropa

 
Michuano ya ligi ya Uropa ilienndelea hapo jana, katika kundi K Tottenham ya uingereza iliivutia chini Anzhi Makhachkala ya urusi huko Moscow kwa mabao mawili kwa bila. Katika Mechi nyingine Swansea ya uingereza iliishinda St Gallen ya uswizi kwa bao moja kwa bila na kuchukua uongozi katika kundi A

Wakati huo huo kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amesema kuwa ije jua ama mvua, kipa wake nambari moja ni Joe Hart. Mlinda lango huyo wa Man City alilaumiwa na wakosoaji wengi katika mechi ya Jumatano dhidi ya Bayern Munich wakisema kuwa uzembe wake uliingia katika ngazi ya juu siku hiyo, na kuicha timu hiyo taabani mikononi mwa Beyern iliyoicharaza mabao matatu kwa moja katika michuano ya klabu bingwa ulaya.

Wakati Mashabiki wa Man City wakiuma vidole vyao kuhusu utendakazi wa kipa wao, wapo baadhi ya Mashabiki wa Man U nao wanaosema kocha David Moyes ameshindwa kazi lakini wamekumbushwa na mtangulizi wake Sir Alex Fergeson kuwa Moyes anatosha. Ikiwa hilo ni kweli au la itajulikana, viwanjani ila kwa sasa Man U inashikilia nafasi ya kumi na mbili katika msimamo wa ligii ya Uingereza jambo ambao limewaacha wengi kujiuliza hatima ya Man U wanaotetea taji hilo.

Na katika riadha mshindi wa mara mbili wa mbio za mita mia mbili Mjamaica Veronica Campbell-Brown sasa yuko salama lakini ameonywa na usimamizi wa ridha nchini humo dhidi ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku. Campbell-Brown ambaye awali alipigwa marufuku Juni baada ya kukataa kuchunguzwa katika kikao kimoja cha riadha Mei, alikabiliwa na jopo la watu watatu lililobuniwa kumchunguza na kumwadhibu.

1 comments:

Raphael Da Silva said...

we are waitn nu'things..