Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, September 24, 2013

Uefa yapingana na kombe la dunia 2022

Raisi wa Fifa Sepp Blatter

Kombe la dunia lipangiwa kufnyika Qatar 2022

Hali ya ati ati kuhusu dimba la kombe la dunia mwaka 2022 na wapi lifanyike , imechukua mkondo mpya baada ya viongozi wa soka Ulaya kukubali kuwa dimba hio haliwezi kuchezewa nchini Qatar wakati wa majira ya joto.

Nchi hiyo ilipata nafasi ya kuandaa michuano hiyo kwa njia ambayo wengi wamepinga ikisemekana viwango vya joto nchini Qatar vinaweza kufika nyuzi hamsini majira ya joto.

Wanachama 54 wa shirikisho la Uefa waliunga mkono hatua hiyo wakati wa mkutano wao nchini Croatia.

"tulichaofikana katika mkutano huu ni kuwa michuano ya kombe la dunia haiwezi kuchezewa nchini Qatar wakati wa majira ya joto" alisema naibu rais wa shirikisho la soka duniani FIFA nchini Uingereza, Jim Boyce.

"kila mtu alikubaliana na wazo hilo.''

Greg Dyke: aliongeza kuwa "michuano hii haiwezi kuandaliwa wakati wa majira ya joto nchini Qatar.''

Kwa mujibu wa Boyce, mjadala wa sasa ni ikiwa dimba hilo lifanyika Januari 2022 au mwezi Novemba ama Disemba mwaka huo.

Mashirikisho ya Uingereza yanalinda maslahi yao yakisema kuwa yanataka kuhakikisha kuwa dimba hilo halihitilifiani na mechi za ligi ya Uingereza wakati Uefa inapendekeza ifanyike Januari ili isiweze kuathiri ligi ya mabingwa wa Ulaya .

Hata hivyo wanasisitiza kuwa hawataki FIFA kuharakisha uamuzi huo.

"bado kuna miaka tisa mbele yetu na watu wanhisi kuwa ni sawa kwa FIFA kukaa na washika dau kujadiliana kuhusu swala hilo na kuwa na mwafaka ambao hautaathiri ligi nyinginezo,'' alisema Boyce

0 comments: