Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, September 19, 2013

Chelsea yala kipigo dhidi ya Fc Basel


Jana ilikua huzuni kwa Jose Mourinho na mashabiki wa Chelsea baada ya kuchapwa nyumbani kwa bao 2-1 na klabu ya FC Basel ya Uswisi.
Hili ni balaa kwa Mourinho kwani hichi ni kipigo cha pili mfululizo ndani ya siku chache kufuatia kupoteza mchezo wikiendi iliyopita kwenye Ligi na Everton.
Chelsea walianza siku vizuri kwa kutangulia kufunga kwa bao zuri la Oscar katika dakika za mwishoni za kiipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili hakikua kizuri kwa Chelsea kwani FC Basel walikuja juu na kujipatia bao mbili katika dakika ya 71 na ile ya 82. Bao hizo zilikwamishwa kimiani na Mohamed Salah, Kijana wa Egypt, na Marco Streller.

VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Oscar, van Ginkel , Lampard, Willian, Eto'o, Hazard
Akiba: Schwarzer, Mata, Mikel, De Bruyne, Ba, Terry, Azpilicueta.

Basel: Sommer, Voser, Schar, Ivanov, Safari, Salah, Diaz, Frei, Stocker, Sio, Streller
Akiba: Vailati, Philipp Degen, Ajeti, David Degen, Delgado, Sauro, Xhaka.
Refa: Daniele Orsato (Italy)

0 comments: