Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, September 27, 2013

THEO WALCOTT KURUDIA UPASUAJI OKTOBA 19

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema operesheni ya tumbo ya Theo Walcott imekwenda vizuri na anatarajiwa kurudi Uwanjani kucheza Mechi ya Ligi Kuu England hapo Oktoba 19.

Upasuaji huo uliyofanywa juzi Jumatano kwa mafanikio, Theo alianza kusikia maumivu ya tumbo wakati alipokuwa akifanya mzoezi mepesi ya kujiandaa kuanza mechi na Stoke City ya Ligi juma lililopita na kitu kilichopelekea kuondolewa katika kikosi cha ikabidi aondolewe kwenye orodha ya watakaoshiriki mchezo huo.

Kwa upasuaji huo Walcott atakosa michezo muhimu ya timu yake ya taifa ya England za Kundi H za Mchujo wa Kombe la dunia dhidi ya Poland na Montenegro dimbani Wembley zitakazochezwa Oktoba 11 na 15.

Winga huyo aliichezea England mechi zake mbili zilizopita za Kundi H za Mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Moldova, ambayo walishinda 4-0 na sare ya 0-0 na Ukraine.

0 comments: