Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, September 19, 2013

Staa wa filamu wa Ghana, Van Vicker atua Dar kushoot movie

Staa wa filamu wa nchini Ghana, Van Vicker wiki hii ametua nchini nchini kwa mwaliko wa kuja kuigiza filamu. Vicker ambaye ni kipenzi cha akinadada ataigiza kwenye filamu moja na Hashim Kambi.

Van Vicker akiwa kwenye Mgahawa wa Akemi, Dar es Salaam

Kupitia Facebook, Kambi amefafanua kuhusu ujio wa staa huyo:

“Tangu jana nimepata simu nyingi kuulizwa kama yanayozungumzwa ni kweli, napenda nitamke kwa furaha sana kuwa yule muigizaji nyota wa afrika magharibi anayetokea ghana yuko hapa tanzania kwa kufanya kazi na mimi kama ambavyo yeye aliniita ghana mwezi wa 2. Hivi tuko location tunaendelea na shooting na mtaziona picha zake muda si mrefu. Nimetimiza ahadi yangu ya kuhakikisha kuwa namleta hapa Bongo na ana furaha sana. Wengine ambao wanashiriki katika movie hii ninayocheza na Van Vicker ni Irene Paul, Slim Omari, Sandra na Weru Sengo. Natumaini ndugu na marafiki zangu nanyi mtaungana nami katika kumuomba zaidi mwenyezi Mungu.”

Vicker alipiga picha hii ya mandhari ya Dar na kupost kwenye Instagram

Lulu akiwa na Van Vicker

Story via Bong5.com

0 comments: