Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, September 17, 2013

FRANCIS CHEKA AAMUA KURUDI DARASANI

Bondia Francis Cheka aamua kurudi darasani, jumatatu ijayo ni siku maalum sana kwa bondia Francis Cheka aliyeitoa kimasomaso Tanzania hivi karibuni baada ya kumtwanga kwa pointi Mmarekani Phill Williams 'The Drill' na kutwaa ubingwa wa WBF uzito wa kati pale Diamond Jubilee Hall. Cheka, ataanza rasmi pre-form one katika shule ya St. Joseph huko Morogoro, akisomea masomo ya Kiingereza na Biashara.
Akizungumzia hilo, Cheka amesema "Sikupata elimu nzuri nikiwa mdogo kutokana na matatizo ya kifamilia, lakini sasa nitaitumia nafasi hii kujiendeleza zaidi".

0 comments: