Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, February 19, 2014

Wyre Kupambana na Jay Z,50 Cents,Asap Rocky na Pharell kwenye World Music Awards



Mkali wa miondoko ya Reggae na R&B kutoka Kenya, Wyre the Love Child, anaendelea kufanya vizuri na kupaisha vizuri Afrika Mashariki ambapo mwaka jana 2013 aliweza kuibuka mshindi katika kipengele cha "Best New Entertainer – Wyre" kwenye tuzo za International Reggae and World Music Awards (IRAWMA) zilizofanyika huko Lauderdale, Florida. 
Kazi za Wyre zimeendelea kufanya vizuri pia mwaka huu na kuvuka zaidi kimataifa na kumpelekea kuwa nominated katika tuzo zenye uzito wa hali ya juu za World Music Awards (WMA) katika kipengele cha World Music Artiste na kikubwa zaidi ni ameshindanishwa na wasanii nguli katika music duniani akiwemo Jay Z,50 Cent,Asap Rocky,Pharell na wengine wengi.. Hii inaonyesha wazi kukuwa kwa muziki wa Afrika Mashariki na kueleweka Duniani kote.. 

0 comments: