Tuesday, February 18, 2014
Bebe ajipanga kuonyesha maajabu kwenye kazi zake mpya
Msanii Bebe Cool, ameamua kuwekeza nguvu ya kutosha katika kazi zake mpya, ambapo ameonekana akitumia vifaa vya kisasa kabisa katika kutengeneza video yake mpya ya ngoma inayofahamika kama Nkola Byafaayo.
Katika video hii, Bebe Cool ameonekana kujipanga vilivyo kuanzia mavaazi yake location mpaka aina za kamera alizotumia kwaajili ya kuleta maana halisi ya jina la wimbo huu kwa kiswahili, Nkola Byafaayo, 'fanya maajabu'.
Bado msanii huyu hajaweka wazi kitita cha pesa alichounguza kufanya video hii, ila amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa itakamilika hivi karibuni tayari kwa kuwachangaza na kuwaburudisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment