Taasisi ya marehemu Steven Kanumba ijulikanayo kwa jina la Kanumba The Great Foundation itazinduliwa rasmi Aprili 7 kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala,jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka miwili tokea kufariki kwa marehemu Kanumba ambaye alifariki dunia Aprili 7.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa
alisema kuwa wameamua kuanzisha taasisi hiyo ili kuendelea kumuenzi
mtoto wake na kuendeleza kile ambacho alikuwa akikifanya wakati wa uhai
wake. Pia aliongezea kwa kusema kuwa
taasisi hiyo itajihusisha na utoaji wa elimu, kusaidia watoto yatima,
kuibua vipaji vya waigizaji chipukizi na kuviendeleza na mambo mbali
mbali ya jamii na tasnia ya filamu na muziki.
“Kwa
njia hii, jamii itaendelea kumkumbuka kila siku na si kusubiri
maadhimisho ya siku yake aliyokufa tu, siku hii (Aprili 7 kila mwaka)
itabaki kuwa ya kukumbukwa, lakini tutajihusisha na mambo mengine ya
maendeleo na kusaidia jamii,” alisema Mama Kanumba.
Alisema
kuwa wameamua kuipa jukumu kampuni ya Vannedrick Tanzania Limited
kufanya shughuli za uzinduzi wa taasisi hiyo kutokana na uadilifu wao na
kuvunia na jinsi inavyojihusisha na mambo mbali mbali katika jamii.
Mkurugenzi kuu wa Vannedrick Tanzania Limited Frederick Mwakalebela
alisema kuwa siku hiyo mbali ya kuwa na Red Carpet, pia kutakuwa na
burudani mbali mbali za muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya na
vichekesho kutoka kwa wasanii maarufu hapa nchini. Alisema kuwa kutakuwa na maonyesho ya filamu mbali mbali za marehemu Kanumba ikiwa pamoja na script alizokuwa akiandika yeye mwenyewe, nyimbo alizotunga na vingienvyo. “Pia
kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Movie ambao wameanza
maandalizi kwa ajili ya siku hiyo maalum kwa waigizaji na mashabiki wa
filamu nchini, tunawamba wadhamini wajitokeze ili kufanikisha siku hiyo,” alisema Mwakalebela.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment