Mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie amesema kuwa yuko tayari kuongeza muda wa mkataba wake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, amekuwa akihusishwa na madai ya kutaka kukihama klabu hiyo kwa kuwa hana uhusiano mwema na kocha wa David Moyes na kumekuwa na fununu kuwa huenda akaondoka mwishoni mwa wa msimu huu. Lakini mchezaji huyo kutoka Uholanzi amesema kuwa anaridhika kucheza chini ya Moyes.
0 comments:
Post a Comment