Shirikisho la Soka Tanzania Tanzania (TFF), limefikia makubaliano na Kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
Kutokana na makubaliano hayo, TFF imepatiwa vifaa kadhaa vya Adidas kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars).
“Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki
dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5, mwaka huu jijini Windhoek,”
ilieleza taarifa ya Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura jana Dar es Salaam.
Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
TFF tunaishukuru Kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini,” alisema Wambura.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment