Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, November 14, 2013

Albam ya Eminem ‘MMLP2′ yauza kopi 792,000 kwenye wiki ya kwanza.

 

Albam ya Eminem "The Marshall Mathers LP 2" imeshika nafasi ya pili mwaka 2013 ya albam zilizouza zaidi kwenye wiki ya kwanza katika chart ya Billboard 200.
‘MMLP2’ imeuza kopi 792,000, ikiwa ni zaidi ya kopi 750,000, iliyokuwa imekadiriwa awali. Msanii pekee ambaye amemzidi mwaka huu ni Justin Timberlake, ambaye albam yake ‘20/20 Experience’ iliyotoka mwezi March na kuuza kopi 968,000.
Kwa idadi ya kopi hizo, Slim Shady ameizidi ‘Nothing Was the Same’ ya Drake iliyouza kopi 658,000. Albam yake ya mwaka Recovery, iliuza kopi 741,000.
Wiki iliyopita, Eminem alikuwa msanii wa kwanza tangu the Beatles mwaka 1964 kuwa na single 4 kwenye top 20.

0 comments: