Eto'o aki'sign mkataba mbele ya katibu na mkurugenzi wa klabu ya Chelsea,David Barnard.
Chelsea imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o kutoka klabu ya Anzi Makhachkala ya Urusi.
Samuel Eto'o,32, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Chelsea.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho, aliamua kumsajili Eto'o baada ya maombi yake ya kumsajili nyota wa Manchester United Wayne Rooney kukataliwa. Mapema wiki hii, ilibainika kuwa Rooney hakuwa tayari kulazimisha uhamisho wake kwa kuwasilisha ombi lake la kutaka kuondoka na hivyo kuzima matumaini ya Chelsea ya Kumsajili mchezaji huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment