Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, March 19, 2014

Yanga na Azam Kuzichapa Leo

Klabu za Yanga na Azam FC leo zitakabiliana katika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara ambayo kimsingi itaweka wazi nafasi ya ubingwa kwa timu zote mbili baada ya dakika 90 kumalizika.
Yanga Sc ambao ni mabingwa watetezi wa soka la Tanzania Bara, wako pointi nne nyuma ya Azam FC inayoongoza kwa kuwa na pointi 43, lakini vijana wa Jangwani wakiwa wamecheza mechi moja pungufu. Azam imeshuka dimbani mara 19 wakati Yanga imeshuka mara 18.
Mbeya City ni wa tatu kwa kuwa na pointi 39 sawa na Yanga, lakini wakiwa na wastani mdogo wa mabao ya kufunga na kufungwa kulinganisha na kikosi cha Hans van de Pluijm.
Yanga imejichimbia Bagamoyo mkoani Pwani baada ya mechi yake ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja
wa Jamhuri Morogoro ambako walitoka sare ya kutofungana.
Kwa upande wake, Azam FC inayonolewa na raia wa Cameroon, Joseph Omog, ilipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya
Coastal Union kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi.
Yanga inaingia uwanjani ikifahamu kuwa ilipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Azam FC kwa mabao 3-2, hivyo si tu itataka kushinda ili kurejesha matumaini ya kutetea ubingwa wake, ila kulipiza kisasi.
Kocha wake, Pluijm amekaririwa akisema kuwa mechi ya leo ni kama fainali, kwani wakipoteza watakuwa wamepata pigo kubwa
katika kuelekea kwenye mbio za kurejesha taji Jangwani.

Rick Ross aamua kupunguza uzito wa mwili


Msanii Rick Ross kutoka pande za Marekani ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kubadilisha aina ya maisha yake ili aweze kupunguza uzito mkubwa wa mwili alionao. Rick Ross ameamua kuchukua uamuzi huo uli kujiweka mbali na magonjwa mbalimbali yanayowakuta watu wenye uzito mkubwa kama presha.

Miaka miwili iliyopita Rick Ross alishawahi kuzimia ghafla akiwa katika ndege, hadi kusababisha ndege hiyo kutua kwa na msanii huyo akakimbizwa hospitali.  Baada ya kufanyiwa uchunguzi iligundulika kua uzito mkubwa alionao pamoja na kukosa usingizi ndio kilikua chanzo cha yeye kupoteza fahamu.

Baada ya hali hiyo ameamua kubadili mfumo mzima wa maisha yake ambapo anafanya mazoezi mara mbili kwa siku, huku akila chakula kwa ajili ya afya na kupata muda wa kupumzika.

Tuesday, March 18, 2014

Rapper Kanye West Apewa Adhabu Kali


Rapper Kanye West akiri mashitaka ya kumshambulia mpiga picha katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Los Angeles. Mpiga picha Paparazzi ,Daniel Ramos, alimtuhumu muimbaji huyo kwa kumpiga makonde na kumpokonya kamera yake. "nilikuwa nafanya kazi yangu wakati Kanye aliponishambulia, '' alisema mpiga picha huyo, '' ingekuwa ni mimi ningekuwa nimemfanyia kitendo hicho ningekuwa kizimbani.''

Mahakama imetoa Adhabu kwa muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36 kuwa  "ni kifungo cha nje cha miaka miwili na ameshurutishwa na mahakama kupata ushauri nasaha kuhusu anavyoweza kudhibiti hasira. Pia ametakiwa kuhudumia jamii kwa masaa 250 kwa kosa hilo alilofanya Julai mwaka jana".




Mpiga picha huyo anadai kuwa bado anatumia dawa kwa ajili ya majeraha aliyoyapa kutokana na kushambuliwa na West. Rapper Kanye alikamatwa mwaka 2008 kufuatia vurumai lengine na mpiga picha katika uwanja huohuo wa ndege. Kesi hiyo, ilitupiliwa mbali na mahakama baada ya West kuwalipia vifaa vilivyoharibika na pia kupata ushauri nasaha kuhusu namna ya kudhibiti hasira zake.

Mali Mpya Kutoka LIN COLLECTION

New arrivals at LIN COLLECTION....Handbags and Shoes..wahi mapema piece ni chache na za ukweli...piga 0767 898471 or Visit Facebook page www.facebook.com/LIN.Collection13



Friday, March 14, 2014

[Photo] Utengenezwaji wa Video Mpya ya Young Money

Tazama picha za kundi la Young Money likiongozwa na Lil Wayne,Nicki Minaj,Tyga, na wasanii wengine kibao,wakiwa kwenye utengenezwaji wa video ya wimbo mpya wa  Young Money "Tyga, Nicki Minaj & Lil Wayne" – Senile kutoka kwenye album yao mpya ya Rise Of The Empire.
111
81
19
26
55 (1)
73

Exclusive Kutoka LIN COLLECTION @Sinza.

Kwa wale wajanja wa Town, Jipatie Handbags,Sandals,Shoes kaliii toka (Thailand,Italy,Northern Europe), Tembelea LIN COLLECTION iliyopo Sinza Makaburini Bus Station... Kujipatia na Mzigo mkalii.. usikose kutembelea duka hilo ili kujipatia vitu special. Kwa mawasiliano zaidi; 0767 898471














Van Persie Atasaini Mkataba Mpya Man Utd..?

Mshambuliaji wa Manchester UnitedRobin van Persie amesema kuwa yuko tayari kuongeza muda wa mkataba wake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, amekuwa akihusishwa na madai ya kutaka kukihama klabu hiyo kwa kuwa hana uhusiano mwema na kocha wa David Moyes na kumekuwa na fununu kuwa huenda akaondoka mwishoni mwa wa msimu huu. Lakini mchezaji huyo kutoka Uholanzi amesema kuwa anaridhika kucheza chini ya Moyes.

Thursday, March 13, 2014

Afya ya Michael Schumacher Yaleta Matumaini

Michael Schumacher ambaye ni Bingwa wa zamani wa mashindano ya langalanga ya Fomula 1, hivi karibuni amekuwa akionyesha dalili nzuri baada ya madaktari kuanza kumtoa katika hali yake mahututi.
Madaktari bingwa nchini Ufaransa wamekuwa wakifanya juhudi za kumuamsha Schumacher ambaye ni bingwa mara saba katoka katika hali yake ya kupoteza fahamu. Madaktari walimuweka Schumacher katika hali ya kupoteza fahamu ili kuzuia uvimbe katika ubongo wake.
Schumacher mwenye umri wa miaka 45 ambaye ni raia kutoka Ujerumani, alipata majeraha mabaya ya kichwa alipokuwa anashiriki mchezo wa kuteleza kwa barafu mwezi Disemba 29 katika maeneo ya Alps Ufaransa.
Familia ya Schumacher imezungumza na kusifu jitihada za madaktari wa Ufaransa na pia wamesema kuwa hiki ni kipindi kigumu kwao na kuwa hawana budi ila kuwa na subira.
Wachunguzi wanasema kuwa Schumacher hakuwa anaenda kwa kasi kubwa wakati wa ajali hiyo ingawa alianguka alipokuwa akiteleza.
Schumacher alistaafu kutoka katika mashindano ya langa langa mwaka 2012 baada ya kushiriki mwa miaka 19.
Alishinda mataji mawili akiwa na kampuni ya Benetton mwaka 1994 na 1995,kabla ya kuhamia kampuni ya Ferrari mwaka 1996 na kuendelea kushinda mataji mengine matano kuanzia mwaka 2000.

Tuesday, March 11, 2014

Je Bayern Munich Watachezea Kichapo Nyumbani Kwao?

Ikiwa ni muendelezo wa michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya, kutakuwa na mechi mbili ambazo zitazichapa usiku wa leo. Arsenal, inaelekea, Bonn, kutoana jasho na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich ambayo ilishinda mechi ya raundi ya kwanza kwa kichapo cha 2-0 katika uwanja wa Emirates.
Ikiwa ni mchezo wa marudiano, Arsenal itakosa huduma za mcheza kiungo wake Kieran Gibbs ambaye kwa sasa anauguza jeraha la mkuu na mshambulizi Yaya Sanogo, huku mlinda lango Laurent Koscielny ambaye alikuwa akiuguza jeraha la paja anatarajiwa kurejea.
                                  arsena
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, ambaye amesimamishwa kucheza kwa muda baada ya kupewa kadi nyekundu wakati wa mechi ya raundi ya kwanza,naye atachukuliwa nafasi na Lukasz Fabianski .
Ukiangalia kupitia historia ya timu ya Arsenal na Bayern kwa mwaka uliopita Arsenal iliishinda Bayern kwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya marudiano lakini ilibanduliwa nje ya mashindano hayo baada ya kupoteza raundi ya kwanza 3-1.
Katika mechi nyingine ya marudiano leo usiku itakuwa kati ya Atletico Madrid Vs AC Milan. Madrid ilishinda awamu ya kwanza kwa bao moja kwa bila. Mario Balotelli huenda akajumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji kumi na mmoja wa AC Millan, baada ya kuuguza jeraha la mgongo alilopata siku ya Jumamosi dhidi ya klabu ya Unidese.
Atletico nayo inamkaribisha mchezaji wake aliyefunga idadi kubwa ya magoli Diego Costa huku ikijaribu kufunzu kwa robo fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na saba iliyopita.
Na ili kufuzu, mabingwa hao mara saba wa Ulaya ni sharti waandikishe historia ya kuwa timu ya tatu katika historia ya kombe hilo kuwahi kushindwa nyumbani katika mechi ya raundi ya kwanza na ishinde mechi ya marudiano ugenini.

[New Audio] ; Fuse ODG ft Sean Paul - Dangerous Love



Sikiliza nyimbo mpya kutoka kwa msanii wa Nigeria aishie Uingereza, Fuse ODG akiwa amemshirikisha Sean Paul - DANGEROUS LOVE.. https://www.hulkshare.com/gongamx/fuse-odg-ft-sean-paul-dangerous-lo

Waigizaji wa Tanzania wapata somo Tuzo za Africa Magic

Tuzo za Chaguo la Watazamaji wa Afrika Magic zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Lagos, Nigeria, ambazo huandaliwa na MultiChoice Africa kwa ushirikiano na Amstel Malta ilishirikisha tuzo 29 katika shindano hilo.
                                                    index
Nigeria ambao ni wenyeji walizoa tuzo 18, Kenya na Ghana walipata tuzo tano kila moja, Zambia ilipata tuzo moja wakati Tanzania ikiambulia patupu katika tuzo hizo, washiriki wa Tanzania walifunguka kwa kusema wanaamini wamejifunza mengi katika tuzo hizo na watakuwa na matokeo bora mwakani.
                                                       images
Gwiji wa filamu wa Nigeria, Ramsey Nouah amesema anaijua vizuri tasnia ya filamu Tanzania kwa kuwa amekuja nchini mara kadhaa na amefanya kazi na wasanii kadhaa akiwemo marehemu Steven Kanumba.
Anaamini kuwa tasnia ya filamu Tanzania inakuwa kwa kiwango kikubwa, lakini inakumbana na tatizo ambalo pia linaikumba nchi yake ya Nigeria.
“Tatizo lililopo kwa tasnia ya filamu Tanzania ni kwamba waandaaji wanafanya kazi kwa kulipua, hawaangalii ubora, wanachofanya ni kutoa kazi kwa wingi ili kupata fedha za haraka,” alisema Ramsey.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Media for Development International, John Riber ambaye ndiye aliyeandaa filamu ya ‘Siri ya Mtungi’ iliyochaguliwa kugombea tuzo saba katika kinyang’anyiro hicho, alisema Tanzania ina nafasi ya koboresha kazi zake za filamu.
“Nadhani bado tuna nafasi ya kuboresha zaidi kazi zetu za filamu ili kupata matokeo mazuri zaidi hapo baadae,” alisema Riber mara baada ya tuzo hizo.
Rehema Samo aliyechaguliwa katika kundi la wanaotengeneza mwonekano wa wasanii, alifunguka kwa kusema pamoja na kutofanikiwa kushinda tuzo anajivunia uteuzi wake. "Kwa kweli nimefurahishwa sana na kitendo cha kuteuliwa tu kushiriki tuzo hizi. Huu ndio mwanzo, vile vile nachukulia kushindwa kupata tuzo kama changamoto na funzo la kuboresha zaidi kazi zangu," alisema Rehema.
Pia aliongeza kuwa kwa sasa wako kwenye mchakato wa kufanya kazi kwa ubora zaidi ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa katika vifaa, taaluma na kuwa na kuthamini kazi za sanaa.
Musa Mziba ambaye filamu yake ‘Vagabond’ ilichaguliwa kugombea tuzo ya filamu bora ya lugha ya asili – Kiswahili, anasadiki kuwa ubora wa kazi za filamu Tanzania bado ni tatizo.“Nadhani ni muhumu sana tukaangalia ubora wa kazi zetu ili ziweze kulingana na kushindana na kazi za wenzetu. Tutaendelea kufanya maboresho na uwepo wetu hapa Lagos imekuwa ni funzo kuu kwetu,” alisema Mziba.

Monday, March 10, 2014

STARS Yaanza Kutumia Jezi Za ADIDAS

Shirikisho la Soka Tanzania Tanzania (TFF), limefikia makubaliano na Kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
Kutokana na makubaliano hayo, TFF imepatiwa vifaa kadhaa vya Adidas kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars).
                           wambuitctff2(8)
“Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5, mwaka huu jijini Windhoek,” ilieleza taarifa ya Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura jana Dar es Salaam.
Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
TFF tunaishukuru Kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini,” alisema Wambura.

Friday, March 7, 2014

Kanumba The Great Foundation kuzinduliwa rasmi Aprili 7

Taasisi ya marehemu Steven Kanumba ijulikanayo  kwa jina la Kanumba The Great Foundation itazinduliwa rasmi Aprili 7 kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala,jijini Dar es Salaam.
                             kanu
Uzinduzi huo utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka miwili tokea kufariki kwa marehemu Kanumba ambaye alifariki dunia Aprili 7.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema kuwa wameamua kuanzisha taasisi hiyo ili kuendelea kumuenzi mtoto wake na kuendeleza kile ambacho alikuwa akikifanya wakati wa uhai wake. Pia aliongezea kwa kusema kuwa taasisi hiyo itajihusisha na utoaji wa elimu, kusaidia watoto yatima, kuibua vipaji vya waigizaji chipukizi na kuviendeleza na mambo mbali mbali ya jamii na tasnia ya filamu na muziki.
                                      kanu mama
Kwa njia hii, jamii itaendelea kumkumbuka kila siku na si kusubiri maadhimisho ya siku yake aliyokufa tu, siku hii (Aprili 7 kila mwaka) itabaki kuwa ya kukumbukwa, lakini tutajihusisha na mambo mengine ya maendeleo na kusaidia jamii,” alisema Mama Kanumba.
Alisema kuwa wameamua kuipa jukumu kampuni ya Vannedrick  Tanzania Limited kufanya shughuli za uzinduzi wa taasisi hiyo kutokana na uadilifu wao na kuvunia na jinsi inavyojihusisha na mambo mbali mbali katika jamii.
Mkurugenzi kuu wa Vannedrick Tanzania Limited Frederick Mwakalebela alisema kuwa siku hiyo mbali ya kuwa na Red Carpet, pia kutakuwa na burudani mbali mbali za muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya na vichekesho kutoka kwa wasanii maarufu hapa nchini. Alisema kuwa kutakuwa na maonyesho ya filamu mbali mbali za marehemu Kanumba ikiwa pamoja na script alizokuwa akiandika yeye mwenyewe, nyimbo alizotunga na vingienvyo. Pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Movie ambao wameanza maandalizi kwa ajili ya siku hiyo maalum kwa waigizaji na mashabiki wa filamu nchini, tunawamba wadhamini wajitokeze ili kufanikisha siku hiyo,” alisema Mwakalebela.