Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, March 19, 2014

Yanga na Azam Kuzichapa Leo

Klabu za Yanga na Azam FC leo zitakabiliana katika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara ambayo kimsingi itaweka wazi nafasi ya ubingwa kwa timu zote mbili baada ya dakika 90 kumalizika.
Yanga Sc ambao ni mabingwa watetezi wa soka la Tanzania Bara, wako pointi nne nyuma ya Azam FC inayoongoza kwa kuwa na pointi 43, lakini vijana wa Jangwani wakiwa wamecheza mechi moja pungufu. Azam imeshuka dimbani mara 19 wakati Yanga imeshuka mara 18.
Mbeya City ni wa tatu kwa kuwa na pointi 39 sawa na Yanga, lakini wakiwa na wastani mdogo wa mabao ya kufunga na kufungwa kulinganisha na kikosi cha Hans van de Pluijm.
Yanga imejichimbia Bagamoyo mkoani Pwani baada ya mechi yake ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja
wa Jamhuri Morogoro ambako walitoka sare ya kutofungana.
Kwa upande wake, Azam FC inayonolewa na raia wa Cameroon, Joseph Omog, ilipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya
Coastal Union kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi.
Yanga inaingia uwanjani ikifahamu kuwa ilipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Azam FC kwa mabao 3-2, hivyo si tu itataka kushinda ili kurejesha matumaini ya kutetea ubingwa wake, ila kulipiza kisasi.
Kocha wake, Pluijm amekaririwa akisema kuwa mechi ya leo ni kama fainali, kwani wakipoteza watakuwa wamepata pigo kubwa
katika kuelekea kwenye mbio za kurejesha taji Jangwani.

0 comments: