Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, March 11, 2014

Waigizaji wa Tanzania wapata somo Tuzo za Africa Magic

Tuzo za Chaguo la Watazamaji wa Afrika Magic zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Lagos, Nigeria, ambazo huandaliwa na MultiChoice Africa kwa ushirikiano na Amstel Malta ilishirikisha tuzo 29 katika shindano hilo.
                                                    index
Nigeria ambao ni wenyeji walizoa tuzo 18, Kenya na Ghana walipata tuzo tano kila moja, Zambia ilipata tuzo moja wakati Tanzania ikiambulia patupu katika tuzo hizo, washiriki wa Tanzania walifunguka kwa kusema wanaamini wamejifunza mengi katika tuzo hizo na watakuwa na matokeo bora mwakani.
                                                       images
Gwiji wa filamu wa Nigeria, Ramsey Nouah amesema anaijua vizuri tasnia ya filamu Tanzania kwa kuwa amekuja nchini mara kadhaa na amefanya kazi na wasanii kadhaa akiwemo marehemu Steven Kanumba.
Anaamini kuwa tasnia ya filamu Tanzania inakuwa kwa kiwango kikubwa, lakini inakumbana na tatizo ambalo pia linaikumba nchi yake ya Nigeria.
“Tatizo lililopo kwa tasnia ya filamu Tanzania ni kwamba waandaaji wanafanya kazi kwa kulipua, hawaangalii ubora, wanachofanya ni kutoa kazi kwa wingi ili kupata fedha za haraka,” alisema Ramsey.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Media for Development International, John Riber ambaye ndiye aliyeandaa filamu ya ‘Siri ya Mtungi’ iliyochaguliwa kugombea tuzo saba katika kinyang’anyiro hicho, alisema Tanzania ina nafasi ya koboresha kazi zake za filamu.
“Nadhani bado tuna nafasi ya kuboresha zaidi kazi zetu za filamu ili kupata matokeo mazuri zaidi hapo baadae,” alisema Riber mara baada ya tuzo hizo.
Rehema Samo aliyechaguliwa katika kundi la wanaotengeneza mwonekano wa wasanii, alifunguka kwa kusema pamoja na kutofanikiwa kushinda tuzo anajivunia uteuzi wake. "Kwa kweli nimefurahishwa sana na kitendo cha kuteuliwa tu kushiriki tuzo hizi. Huu ndio mwanzo, vile vile nachukulia kushindwa kupata tuzo kama changamoto na funzo la kuboresha zaidi kazi zangu," alisema Rehema.
Pia aliongeza kuwa kwa sasa wako kwenye mchakato wa kufanya kazi kwa ubora zaidi ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa katika vifaa, taaluma na kuwa na kuthamini kazi za sanaa.
Musa Mziba ambaye filamu yake ‘Vagabond’ ilichaguliwa kugombea tuzo ya filamu bora ya lugha ya asili – Kiswahili, anasadiki kuwa ubora wa kazi za filamu Tanzania bado ni tatizo.“Nadhani ni muhumu sana tukaangalia ubora wa kazi zetu ili ziweze kulingana na kushindana na kazi za wenzetu. Tutaendelea kufanya maboresho na uwepo wetu hapa Lagos imekuwa ni funzo kuu kwetu,” alisema Mziba.

0 comments: