Eto'o aki'sign mkataba mbele ya katibu na mkurugenzi wa klabu ya Chelsea,David Barnard.
Chelsea imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o kutoka klabu ya Anzi Makhachkala ya Urusi.
Samuel Eto'o,32, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Chelsea.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho, aliamua kumsajili Eto'o baada ya maombi yake ya kumsajili nyota wa Manchester United Wayne Rooney kukataliwa. Mapema wiki hii, ilibainika kuwa Rooney hakuwa tayari kulazimisha uhamisho wake kwa kuwasilisha ombi lake la kutaka kuondoka na hivyo kuzima matumaini ya Chelsea ya Kumsajili mchezaji huyo.
Friday, August 30, 2013
Thursday, August 29, 2013
FUSE ODG IN DAR-AZONTO LIVE SEPTEMBER 7.
Jux kuzindua video yake iliyofanyika China
MISS TANZANIA 2012/2013 BRIGITTE ALFRED AAGWA RASMI USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA HOTELI YA GIRAFFE
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akitoa nasaha zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2013,wakati wa hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu ya kumuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World).Hafla hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko na kushoto ni Mlezi na shoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko (pili kulia),Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) pamoja na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es Salaam usiku huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza machache ikiwa ni pamoja na kuwaasa Warembo waliopo kambini hivi sasa kujitahidi kufanya vyema.
Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza.
Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dkt. Charles Bekoni akitoa salamu.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akikumbatiana na Mama yake Mzazi wakati wa Kumuaga.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akitoa shukrani zake wakati wa hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa kwenye hafla hiyo.
Tuesday, August 27, 2013
Tuesday, August 13, 2013
New Hit:MABESTE FT PETER MSECHU-NISHAURI
Download new hit kutoka kwa Mabeste Ft Peter Msechu-Nishauri,
Produced by Gard/Manecky
AM Records
.http://www.hulkshare.com/dj5mmlq6wcn4.
Produced by Gard/Manecky
AM Records
.http://www.hulkshare.com/dj5mmlq6wcn4.
Friday, August 9, 2013
Mabeste Venance's Blog Inawatakia Eid Mubaraq
Baba Mzazi Wa Rapper Collo Afariki
Rapper Collins Majale a.k.a Collo amepata pigo la kumpoteza Baba yake mzazi. Collo ali'tweet kwenye page yake "There's more to life...Happiness because u did a fantastic job in & on raising us. RIP #papa You forever live in my heart."
Mabeste's Blog inapenda kufikisha rambirambi za dhati kwa Collo na familia yake.
Thursday, August 8, 2013
Picha Za Zawadi Ya Mchumba Wa Peter Okoye Wa P Square.
Msanii Peter Okoye ambaye anaunda kundi la P Square,amzawadia mchumba wake Mrs Lola Natasha gari aina ya Range Rover
Peter akiwa na mchumba wake Lola Natasha.
Mchumba wa Peter wa P Square akionyesha pete aliyopewa na mchumba wake Peter baada ya Engagement.
Vanessa Mdee Baada Ya 'Closer' Anakuja Na Ujio Mpya
Msanii Vanessa Mdee baada ya kufanya vizuri kwenye wimbo wake unaokwenda kwa jina la 'Closer' sasa anakuja na ujio mpya
Hii ni picha wakifanya maandalizi ya cover ya wimbo wake mpya pia alifunguka "Behind the scenes look of what REALLY went down.. Mad love to the Hot in Dar team. @OsseGrecaSinare who's such a professional on the field. My lovers Diana and Yohanna who stay slaying with that BEAT ( make Up ) and amazing hair from"
Lina Sanga Anatarajia Kuja Na Tv Show Yake.
Baada ya Lady Jay Dee,Irene Uwoya,Wema Sepetu,Rose Ndauka na wengineo kuja na vipindi vyao katika luninga,sasa ni zamu ya Lina Sanga. Anatarajia kuja na kipindi kipya kwenye luninga yako hivi karibuni kinachokwenda kwa jina la (3D).
Lina alifunguka hayo kupitia page yake ya instagram kwa kupostpicha na status "#on set..my new tv show{ comingsoon} 3D"
Wednesday, August 7, 2013
Madam Rita Aelezea Sababu Za Kuhamishia Kipindi cha Bongo Star Search Kutoka ITV Kwenda TBC One.
Benchmark Production(CEO) Madam Ritha Paulsen alifunguka kupitia facebook page yake kuwa "Baada ya kusoma maoni yenu, ningependa kufafanua sababu mbili za kurusha Epiq Bongo Star Search 2013 kupitia kituo cha Televisheni cha TBC1.
Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara ndio zimepelekea kipindi cha EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya pili ni kwamba baada ya kwenda kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye ving'amuzi karibia vyote vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku.
Nashukuru sana kwa maoni yenu mlioyatoa na mmesikika. Nawatakieni siku njema!"
Tuesday, August 6, 2013
EID MOS:MABESTE'S NIGHT NDANI YA DAR WEST PARK(TABATA)
#XCLUSIVE EID MOSI
Mabeste's Night..
Ukumbi:Dar West Park (Tabata)
Kiingilio ni 5000/= tu!
Usikose budaaaaaah...
#MuchLove
Subscribe to:
Posts (Atom)